NA
HAJI NASSOR, PEMBA
BAADA
ya mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa kusini Pemba, kughairisha
kumsomea hukumu Oktoba 31, mwaka huu, mwalimu wa skuli ya Madungu, anayedaiwa
kumbaka mwanafunzi, sasa hukumu hiyo inatarajiwa kusomwa leo Novemba 14, mwaka
huu.
Maana Oktoba 31, mwaka huu hukumu
hiyo haikusomwa mahakamani hapo, baada ya Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali
Juma, kusema kuwa, alikuwa hajamaliza maandalizi yake.
Alisema, kuwa kutokana na
kuwepo kwa hukumu nyingi na baadhi ya kesi kuzitolea uamuzi, ndio maana hukumu
ya mtuhumiwa Ali Khatib Makame, nayo ni miongoni ambazo hazijamaliza vizuri.
Hakimu Muumini Ali Juma, alisema wiki iliyopita, (Oktoba 31) alilazimika kughairisha kumsomea hukumu mtuhumiwa huyo,
na kuamua kuipanga asubuhi ya leo.
‘’Ni kweli baada ya
kughairisha kusoma hukumu hiyo, na hasa baada ya kushauriana na upande wa
mashataka na ule wa utetezi, niliamua kulirejesha tena shauri hili asubuhi ya
leo Novemba 14, mwaka huu kwa ajili ya kumsomea hukumu,’’alisema.
Awali Mwendesha Mashataka
kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka, Ali Amour Makame, alidai kuwa shauri
hilo lipo mahakamani hapo, kwa ajili ya hukumu na hasa baada ya pande zote
mbili kufunga ushahidi wao.
Wakili wa mtuhumiwa huyo
Suleiman Omar Suleiman, alipoulizwa na Hakimu Muumini, alidai hana pingamizi
yoyote juu ya uamuzi, uliotolewa mahakamani hapo.
‘’Niko tayari pamoja na
mteja wangu, kuwa leo Novemba 14, iwe ndio siku ambayo mahakama hii chini ya
Hakimu Muumini Ali Juma, kumsomea hukumu mtuhumiwa huyu,’’alidai wakili huyo wa
utetezi.
Ambapo kwa upande wa
utetezi, ulifunga ushahidi wake tokea Oktoba 19, mwaka huu baada ya mtuhumiwa
huyo kuwasilisha mashahidi wanne, wakiwemo waalimu wa skuli ya Madungu msingi.
Kwa upande wa mashtaka,
ukiongozwa wakili wa serikali Ali Amour Makame, ulifunga ushahidi wake tokea
Oktoba 11, mwaka huu na Oktoba 12, mahakama hiyo ikatoa uamuzi, kuwa mtuhumiwa anyo
kesi ya kujibu.
Hivyo kutoka Oktoba 19, mara
baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao, mahakama hiyo maalum ya makosa
ya udhalilishaji, imepanga leo Oktoba 31 iwe ni siku ya kusoma hukumu, ingawa
pia imeghairishwa tena hadi leo Novemba 14, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Ali Makame Khatib (mwalimu wa skuli ya msingi Madungu),
mkaazi wa Matuleni wilaya ya Chake chake, alidaiwa kumbaka mtoto (mwanafunzi
wake) mwenye miaka 11.
Ambapo kufanya hivyo ni
kinyume na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment