NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, amevishauri vilabu ya mazoezi nchini, kujitengenezea kanuni, zitakazowavutia watu wingi zaidi kujiunga kwenye mazoezi, ili kuondoa dhama potofu ya mazoezi ni uhuni. Alisema, kama kundi kubwa la watu wanadhana kuwa mazoezi ni uhuni na kuvunja maadili, ni wakati sasa kwa vilabu vya mazoezi na michezo, kuwa na kanuni zitakazofuta dhana hiyo. Makamu huyo wa Kwanza, aliyasema hayo leo Julai 28, 2024 uwanja wa michezo Gombani Chake chake, kwenye bonanza la miaka 10, tokea kuanzishwa kwa ‘Gombani Fitness Club’ lilioandaliwa kwa pamoja na TAMWA-Zanzibar na Shirika la Bima. Alieleza kuwa, kwa vile mozoezi ni jambo muhimu kwa kila mmoja, ni vyema kuwepo na kanuni ndogo ndogo, ambazo zitawavutia wengine, kushiriki katika kupata kinga ya miili yao. Alifahamisha kuwa, ni kweli kama kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili, inaweza kuwa sababu kwa baadhi ya watu, kuona sio sehemu salama, ingawa zikiwepo