NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, utakaofanyika Aprili 2 mwka huu katika Uwanja wa michezo Gombani Chake Chake Pemba. Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Rashid Hadid Rashid, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2026 ofisini kwake Chake Chake Pemba. Alisema kuwa, katika uzinduzi huo Dk. Mwinyi atahutubia wananchi pamoja na kuzindua rasmi mbio za mwenge wa uhuru na kuendelezwa kwa ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo katika wilaya nne kisiwani Pemba. Alisema, mwenge wa uhuru hukimbizwa nchi nzima ikiwa ni sehemu ya kuenzi uhuru wa taifa, kuenzi maendeleo ya nchi sambamba na kudumisha Amani, mshikamano na maelewano ya wananchi katika shughuli mbali mbali za maendeleo ya taifa. "Mwenge wa uhuru mwaka huu 2026 unatarajiwa kuzinduliwa P...