Joyce Joliga ,Songea
MWALIMU Mkuu shule ya Msingi Halale Gaudence Luambano amesema utoaji wa chakula shuleni umesaidia kupunguza tatizo la utoro wa wanafunzi na hivyo kuweza kuongeza ufahulu.
Hayo ameyasema jana wakati wa mahojiano maalum na mtandao huu ambapo alifafanua zaidi kuwa shuke hiyo inawanafunzi 722 ambao wote wanapata chakula shuleni hapo kutokana na michango ya wazazi wao.
Alisema,wazazi wameajili mpishi ambaye wanamlipa kila mwezi kwa ajili ya kuandaa chakula cha wanafunzi hao pindi wakiwa wanaendelea na masomo yao
" Utoaji lishe mashuleni umechochea sana kupunguza Utoro kwa wanafunzi ,kwani wanahuakika wa kupata chakula hapa hapa shuleni ,hivyo kujikita wakifanya vema kwenye masomo yao:"
Aliongeza kuwa anawashukuru wazazi wenye watoto shuleni hapo kwani wanekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanachangia chakula pamoja na maendeleo ya shule kwa vitendo ili watoto wao waweze kusoma kwenye mazingira mazuri na kupata elimu
Aidha,ameishukuru Halmashauri ya wilaya ya Mbinga kwa kuwajali walimu na kuweka miundo mbinu bora ya kujifunzia na kufundishia .
Naye Benedictor Mbilinyi amewataka wazazi kuendelea kuchangia michango kwa hali na mali ilikuweza kuinua elimu kwani ushirikiano wanaotoa ndio unaosaidia kutia moyo walimu kuendelea kufundisha kwa bidii.
Naye Mwanafunzi pendo Michael (6) wa darasa la pili alisema chakula kimewasaidia kuacha kusinzia darasani kutokana na njaa,pia wamekuwa wakila pamoja kwa upendo .
mwisho
Comments
Post a Comment