Skip to main content

Posts

Showing posts from October 19, 2025

50 KWA 50 YAWATIA JOTO WANAUME KWENYE SAFU YA UONGOZI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ MATAIFA kadhaa ulimwengini, Tanzania ikiwemo zimeridhia mikataba na matamko ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kwenye uongozi.   Hii ni kama ilielezwa katika tamko maarufu la la Haki za Binadamu la mwaka 1948.   Zanzibar imesaini mikataba ya kikanda na kimataifa, lakini safari ya utekelezaji ni ndefu kwa sababu hadhi sawa  kwa wanawake na wanaunme katika uongoz.   Mara nyingi unapofanyika uteuzi nafasi wanazopewa wanawake huwa hazina hadhi sawa na zile wanazokabidhiwa wanaume.   Vyama vya siasa navyo vinawaacha nyuma wanawake katika kuwapa nafasi za kugombea kama, inavofanyika kwa wanaume na jina la mwanamke likipita huwa kama bahati mbaya.     Taarifa ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, inafafanua kuwa, kwa uchaguzi wa 2020, wanaume walioteuliwa na vyama kugombea kuingia katika Baraza la Wawakilishi walikua 190 na walioshinda ni 42 wakati wanawake walikuwa  61 na walioshinda ni wanane (...

ZEC YADAI KULAINISHA MAZINGIRA RAFIKI KWA MAKUNDI MAALUM UPIGAJI KURA

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ TUME ya uchaguzi Zanzibar ‘ZEC’ imesema imeshaandaa mazingira rafiki   kwa watu wa makundi maalumu, wakiwemo   wenye ulemavu, ili kuh’akikisha ushiriki wao, katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu. Hayo yameelezwa na Kamishna wa tume hiyo Pemba Ayubu Hamad Bakar, wakati akizungumza na wadau wa uchaguzi, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano Wawi Chake chake Pemba. Alisema ili kuhakikisha makundi hayo yanashiriki ipasavyo katika uchaguzi huo ‘ZEC" imeweka vituo vya kupigia kura, katika maeneo yanayofikiwa na kila mmoja. Alisema jingine ZEC, imeandaa vitambulisho maalumu kwa watu wenye ulemavu, imetoa mafunzo maalum kwa maafisa wake, yanayozingatia uhitaji wa watu hao pamoja na kuchapisha vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu wa uoni. "Ili kuhakikisha ushiriki wa kila mmoja katika mchakato huu wa kidemokrasia, tumeweka mazingira rafiki kwa kila mmoja, ikiwa ni kuwafundisha maafisa wetu, jinsi ya kutoa huduma...

WAGOMBEA CUF JIMBO LA MTAMBILE KUWANG'ARISHA VIJANA, WANAWAKE KIUCHUMI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAGOMBEA Ubunge na Uwakilishi wa Jimbo la Mtambile kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, wamesema kama wakipewa ridhaa, makundi ya vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na wajasiriamali, watanufaika kwa mikopo isiyo na riba, kama njia ya kuwakwamua na umaskini. Walisema, wameshaona wapi wanaotoa mikopo wanakosea, na kuendelea kuyaacha makundi hayo, wakichukua mikopo ingawa, kisha hurudi tena kwenye hali ngumu ya maisha. Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kampeni za nyumba kwa nyumba jimboni humo, wamesema njia pekee ya kuwapa maisha bora makundi hayo, ni kuwachagua wagombea wa CUF na kisha, kulitekeleza hilo. Mgombea Ubunge jimboni humo Rashid Soud Khamis, alisema, ameshaiona njia ya makundi hayo kuondokana na umaskini wa kipato, ikiwemo ile ya kuwapatia mikopo isiyo na riba. Alieleza kuwa vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na wajasiriamali wa Jimbo la Mtambile, hawaamini kuwa, mikopo yenye riba ni njia ya kufikia ndoto zao, bali wanahi...

VIZIWI WATAMANI KAMPENI JUMUISHI, TAMWA -ZANZIBAR YATOA RAI KWA VYAMA

    NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ ZANZIBAR ipo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mashariki mwa Afrika. Ni miongoni mwa nchi zinazopata viongozi wake kupitia mchakato wa upigaji kura. Ambapo kila baada ya miaka mitano wananchi wake, wenye sifa zilizotajwa kikatiba, hupiga kura ili kuchagua kiongozi wamtakae. Mchakato huo humjumuisha kila mtu, ilimradi awe ametimia miaka 18 na asiwe mwenye changamoto ya ufahamu ama akili. Izingatiwe kwamba, upigaji kura ni haki ya kikatiba ya kila Mzanzibari, kwani katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 7(1) kimetoa haki hiyo. Kwamba ‘’Mzanzibari alietimiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Zanzibar,’’kimefafanua. Kwa kulizingatia hilo, Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC, imeidhinisha jumla ya wazanzibari 717, 557 kushiriki katika uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu. Huku taarifa kutoka tume hiyo zikieleza kwamba, kati ya hao   watu wenye ulemavu 8,021 wanatarajiwa kushiriki katika zo...

VYAMA KUKOSA WAKALIMANI, VIZIWI ZAWAPITA UPANDE SERA, AHADI ZA WAGOMBEA

  NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ VYAMA vya siasa vitambue kuwa kuna watu wenye ulemavu wa uziwi na wana haki ya kusikiliza kampezni zao. Kuna baadhi ya vyama havijazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu, hasa wale wenye uziwi, katika mikutano. Jambo ambalo linalowanyima haki yao ya msingi ya kufatilia sera za vyama, ili siku ya kupiga kura wafanye uamuzi sahihi.      Vipo vyama 17 vilivyosimamisha wagombea na 11 vimefanikiwa kusimamia wagombea urais, ingawa ni chama cha mapinduzi CCM pekee ndio kinachotekeleza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu wa uziwi. Imefahamika vyama vyengine vimekuwa vikiendesha kampeni zao bila ya kuwashirikisha watu wenye ulemavu wa uziwi, kwa kukosekana kwa wakalimani wa lugha za alama. Tena zipo asasi za kiraia kadhaa ikiwemo ile ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), Jumuiya ya Wanasheria wanawake   Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake ...

KATIJA MWENYE ULEMAVU WA VIUNGO, AWATIA HOFU WANAUME, ASEMA 2030 'HAIISHI MPAKA IISHE'

   NA  ARAFA MAKAME, PEMBA@@@@ HAPA ni Kiuyu Minyungwini, wilaya ni ya Wete, mkoa wa kaskazini Pemba, na mbele yangu namuomba mjasiriamali, bila shaka ni mtu mwenye ulemavu wa viungo.   Niliharakia, kutaka kumjua ni nani, nilipomkaribia ana nadisha haya kangaa…kangaaa…na wale wa wapenzi wa madira na vipodozi nipooo.... njooo ujichagulie.   Kauli hizo, zilinifanya nisimame pembeni kidogo mwa nyumba ya Asha Haji Makame wa Kiuyu, nae mjasiriamali huyo, aligeuka nyuma ghafla, kwa hamu ya kutafuta wateja na alinifuata.   …..assalama alyekum, baada ya kuitikia mjasiriamali huyo, alimuuliza bi Asha kua amepata mgeni, na kumjibu ni mgeni wako.   ‘’Au ndio huyo mwandishi wa habari aliyenipigia simu, juzi kuniambia anakuja, nilijua utachelewa kidogo ndio maana, nimeanza kutembeza biashara yangu,’’alisema.   ‘’Kwani wewe ndio Katija Mbarouk Ali, nilikua nawasiliana na wewe bila ya kukufahamu, ndio   nimekuja kukuhoji,’’alidakiza mw...