Skip to main content

Posts

Showing posts from July 5, 2026

RC: KUSINI PEMBA, AKABIDHI RUZUKU KWA WAJASIRIAMALI, AIPA TANO ZNCC

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadid Rashid, amesema jumuiya ya kitaifa ya wafanyabiashara Zanzibar ‘ZNCC’ imekuwa chanzo kikuu cha kuwaonesha njia za kujiajiri vijana, kutokana na juhudi zake mbalimbali. Mkuu huyo wa mkoa, aliyasema hayo leo Julai 11, 2026 ukumbi wa Kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake chake, kwenye hafla ya kukabidhi ruzuku kwa wajasiriamali, kupitia mradi wa ‘ Inclucities’ , unoaendeshwa kwa pamoja na jumuiya hiyo na Trias na Enabel kama mtekelezaji mkuu. Alisema ZNCC, imekuwa ikihangaika huku na kule, ili kuhakikisha wajasiriamali, wanaendelea kujiajiri wakiwa na uhakika wa uwezeshaji, kama mfano wa ruzuku kama hizo zilizotolewa. Alifahamisha kuwa, kwa ZNCC kufanya hivyo, ndio maono ya serikali iliyomadarakani, kuhakikisha wajasiriamali wanawezeshwa kwa njia tofauti. ‘’Kwanza niwapongeze sana wenzetu wa ZNCC kwa kushirikiana na Trias na Enabel, ambapo leo tunashuhudia utoaji wa ruzuku, kwa wajasiriamali wetu,...

'THBUB' YAWAHIMIZA WAZAZI, WALEZI KUVUNJA UKIMYA DHIDI YA UDHALILISHAJI WA WATOTO

NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIBAR@@@@ AFISA Uchunguzi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Ofisi ya Zanzibar, Abdul-latif Ali Sheha amewasihi wazazi na walezi wa Shehiya ya Kinuni, kujenga utamaduni wa kuzilinda na kuziishi haki za watoto kwa vitendo. Abdullatif alitoa nasaha hizo kwa wazazi na walezi 637 katika Madrasatul Thamaraatul Jannah iliyopo Shehia ya Kinuni, Mkoa wa Mjini Magharibi wakati akiwapa hao elimu ya haki za watoto na wajibu wa jamii katika kuzuia vitendo vya ukatili wa watoto na uvunjwaji wa haki za binadamu ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu na msaada wa sheria wakati wa mwendelezo wa zoezi la Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia Awamu ya Pili (MSLAC II) unaoendelea katika Wilaya tatu za Mkoa wa Mjini Magharibi. “Mtoto ana haki ya kuishi katika mazingira salama, kupatiwa elimu na kulindwa dhidi ya aina zote za unyanyasaji" Alisisitiza bw. Abdullatif. Pia aliwaeleza wazazi hao kuwa jamii inapaswa kuachana na tabia ya kuoneana muhali ...

ANGUKO LA UCHUMI LA WANAWAKE HUANZIA HAPA

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ KATIKA zama hizi, wanawake wanakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo utelekezwaji. Ambao kwa kiasi kikubwa, unaathari za moja kwa moja katika uchumi na ustawi wa maisha yao. Mara nyingi, utelekezwaji huo hufanywa na wanaume kutokana na sababu kadhaa, huku wengi wa wanaotelekezwa, wakitupia lawama ndoa za mke zaidi ya mmoja. Katika hili, wanawake wengi waliofanya mahojiano na mwandishi wa makala hii, ambao wamewahi kutelekezwa walisema, chanzo ni ndoa za mke zaidi ya mmoja. Huku Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Wete Salma Saleh Hamad akigongea msumari kuwa, katika idadi ya mashauri ya kesi za utelekezaji wanazopokea ofisini kwao, asilimia 90 yanaonesha chanzo ni ndoa za mke zaidi ya mmoja. NINI UTELEKEZAJI FAMILIA? Ni kule mtu kushindwa kupeleka mahitaji kwa yule unaepaswa kumpa, hali ya kuwa unauwezo wa kutoa mahitaji hayo. Utelekezaji unaweza kuwa wa moja kwa moja au katika huduma za elimu, afya na hata kihisia. Ingawa Serikali na wad...