NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAZIRI wa Uvuvi na Uchumi wa Buluu Zanzibar, Massoud Ali Mohamed, amewataka wananchi kuendelea kuyathamani Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, kwani ndio msingi wa maendeleo yaliopo. Waziri Massoud, alitoa raia hiyo jana, wakati alipomaliza shughuli za ufunguzi wa kituo cha kisasa cha ununuzi wa karafuu, eneo la Kiwani wilaya ya Mkoani Pemba, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 62 ya mapinduzi. Alisema kuwa, mapinduzi sio hadithi ya kuvutia pekee, bali ni kuwepo kwa maendeleo kila sekta, kama ilivyokuwa azma ya waasisi wa taifa hili. Alieleza kuwa, kwa mfano Kiwani iliyokuwepo kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na ya sasa ni tofauti, kwa kuwepo miundombinu ya kisasa, kwenye sekta ya afya, elimu, maji safi na salama na barabara. Alieleza kuwa, hayo ndio thamani na umuhimu wa kufanyika kwa mapinduzi hayo, na sasa ipo haja kwa wananchi na hasa wapenda maendeleo, kuyathamini na kuyaenzi kwa nguvu zao zote. ‘’Niwatake wanan...