NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WATUMISHI wa umma wanaotarajiwa kustaafu wametakiwa kuwa makini wanapopokea ushauri wa watu mbali mbali, ili waepuke kupoteza fedha nyingi bila ya mafanikio. Akifungua mafunzo kwa wastaafu hao watarajiwa, leo Machi 5, mwaka 2025 Afisa Mdhamin Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali alisema, kuna watu wengi watajitokeza kuwapa ushauri wa mambo mbali mbali, hivyo wawe makini katika kuupokea na kuutekeleza. Alisema kuwa, wastaafu bado wana mchango mkubwa kwa taifa, hivyo kuna haja ya kujipanga mapema katika kujitafutia miradi ambayo itaendeleza maisha yao baada ya kustaafu. "Kila mtu atakujia kukushauri kufanya biashara na wingine watakushauri kufanya vitu vyingine, lakini muwe makini ili fedha zenu za kiinua mgongo, zitumike kuwakomboa kimaisha na sio kuwasababishia matatizo," alisema Mdhamini huyo. Aliwataka watumishi hao wayafanyie kazi mafunzo waliyopatiwa, kwani wanakwenda kulitumikia taifa kwa upande mwingin...