NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@ WAALIMU wa skuli kisiwani Pemba, wametakiwa kujenga ushirikiano wa pamoja katika kuwaelimisha wanafunzi, juu ya kupata uwelewa wa mradi wa ‘Eco-Schools’ na kuingiza katika mitaala yao ya kimasomo, ili kupata elimu ya utunzaji wa mazingira. Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa ‘Eco-Schools’ Talib Kassim Abdi kwenye mafunzo ya utunzaji wa mazingira, kwa walimu hao, waliomo katika mradi huo, yaliyofanyika ukumbi wa TASAF Chake chake Pemba. Alisema, ipo haja kwa waalimu hao kuyatumia mafunzo hayo, yatokanayo na mradi huo, kwani yatawajengea uwelewa, wakati wa kuwafundisha wanafunzi, mada zinazo za utunzaji na athari za kimazingira zitokanazo na mabadiliko tabia nchi. Mapema akifungua mafunzo hayo ya siku mbili, Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa wa kusini Pemba, Mohamed Shamte Omar, alisema utekelezaji wa mpango huo, ni fursa kwa wanafunzi kuzipatia ufumbuzi changamoto za kimazingi...