NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ACHA kufukua makaburi, kujua yaliopita kwa siasa za Pemba. Maana chaguzi sita za vyama vingi, zilizokwishapita, ukiamua kufuakua makaburi, wapo watakolia, watakaofuta machozi na wingine kupoteza fahamu. Acha kabisa, kuuliza, kufungua ripoti, kusaka takwimu, kuingia kwenye mitandao ya kijamii au kusililiza rikodi, za maovu yaliopita. Wewe jua tu, kuwa taifa la Tanzania tokea pale lilipofanya uchaguzi wa kwanza mwaka 1995, sasa linaingia uchaguzi mkuu wa saba Oktoba 29, mwaka huu. Narejea tena, acha kabisa kutaka kujua siasa za Pemba, jinsi zilivyokuwa na nguvu hadi kupindukia mipaka, tena ndani miezi kama hii ya kmapeni. SIASA ZA MWAKA HUU ZINATOFAUTI GANI? Juzi nilishuhudia siasa za kiungwana, kistaarabu na za kisheria, kwa wafusia wa vyama vya CCM kubishana kwa hoja za sera, na wenzao wa ACT-Wazalendo. ‘’Huyu Dk. Mwinyi anafaa, maana kwanza ni daktari atawafanyia uchunguuzi na kisha kuwatibu nyote...