NA HANIFA SALIM, PEMBA@@@@ AFISA Mdhamini wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto Pemba Hafidh Ali Mohamed, amewataka waandishi wa habari watumie kalamu zao katika kuelimisha jamii juu ya ulipaji wa kodi na matumizi sahihi ya risiti za elektroniki. Alisema kuwa, waandishi wa habari ndio daraja la mawasiliano hivyo, ni vyema kuitumia taaluma yao ya uwandishi wa habari katika uwandaaji wa makala na vipindi vya kila siku kwa lengo la kuielimisha jamii. Aliyasema hayo alipoua akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, huko ukumbi wa TASAF Chake chake uliyoandaliwa na klabu ya waandishi wa habari wa Pemba (PPC) kwa ufadhili wa mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA. "Maadhimisho haya ni muhimu na elimu mutakayoipata hapa itasaidia sana kuwajengea uwelewa juu ya masuala ya kodi, yatawasaidia kuandika habari za kweli, zenye uweledi na zilizofanyiwa utafiti wa kutosha, naomba tuyatumie mafunzo haya kwa vitendo", alis...