SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imepandisha bei ya karafuu kutoka shilingi 14000 hadi shilingi 15000 kwa kilo moja ya Daraja la Kwanza kwa mwaka 2023-2024. Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na kufunguliwa kwa vituo vya kununulia karafuu kwa Unguja na Pemba katika ofisi za Wizara hiyo Kinazini. Alisema Shirika la Biashara la Taifa litafungua vituo mbali mbali vya kuauzia karafuu kuanzia tarehe 3 mwezi huu Unguja na Pemba hivyo amewataka wananachi kuuza karafuu zote katika Shirika hilo la Biashara la Taifa ZSTC. Alifahamisha kuwa kwa hatua ya awali shirika litaanza kufungua kituo cha Saateni kwa Unguja na kwa upande wa Pemba watatumia Kituo cha Mkoani,Madungu na Bandarini Wete kuuzia zao hilo na kauahidi kuongeza kufungua Vituo vyengine kulingana na mahitaji. Akizungumzia suala la malipo kwa wakulima wazao hilo alisema shirika limejipanga kuwalipa wananchi hapohapo kwa mfumo wa Kielektroniki k