NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MGOMBEA Uwakilishi Jimbo la Chambani wilaya ya Mkoani, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Bahati Khamis Kombo, amesema kama akipata tena ridhaa, kundi la wanawake wajane na vijana, atawaimarishia miundombinu ya kujiwezesha kiuchumi. Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya uzinduzi wa kampeni eneo la Dodo Pujini, alisema kupitia Ilani ya CCM, mikakati yake, ni kuona na kundi hilo analiwezesha. Alisema, ndani ya jimbo hilo, anajua kuwa wapo vijana wasiokuwa na ajira na wale wajane walionyimwa haki zao kwa njia moja ama nyingine, hivyo nia yake ni kuwawezesha. Alieleza kuwa moja ya mbinu atakazotumia ni kuwapa taaluma ya ujasiriamali na kuwatafutia mikopo, ambayo itakuwa chachu ya kuendesha maisha yao. Alisema njia nyingine ni kuwawezesha kwa kazi za mikono, kama kufuma na kushona, ili iwe njia sahihi ya kufikia ndoto zao. ‘’Hapa ninacho hitaji kutoka kwa wananchi wa jimbo hili, kwanza waweke kando tofauti za vyama, wanipe ...