NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAANDISHI wa habari na wana asasi za kiraia Pemba, wametakiwa kufanyakazi kama mwili mmoja, ili wanapofuatilia kero za wananchi, iwe kazi rahisi kuzipatia ufumbuzi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ Mohamed Najim Omar, wakati akiufungua mkutano wa siku moja, kwa waandishi hao wa habari na wanaasasi za kiraia Pemba, mkutano uliofanyika leo Juni 21, 2024 ukumbi wa Maktba Chake chake. Alisema, waandishi wa habari na wanaasasi za kiraia, imegundulika wote wanawatetea wananchi wanaokabiliwa na changamoto, mfano ya ukosefu wa barabara, hivyo ni vyema wakashirikiana katika hilo. Katika hatua nyingine Najim, alisema ushirikiano kati ya pande mbili hizo, unaweza hata kubadilisha sera na sheria, ambazo zinaonekana kupitwa na wakati, katika uendeshaji wa shughuli zao. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ‘PACSO’ Sifuni Ali Haji, alisema anategemea baada ya kumalizika kwa mradi huo, kuweko na mabadiliko makub