NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ DISEMBA 3 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu. Siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka 1992 na umoja wa mataifa, lengo likiwa ni kuongeza uwelewa juu ya mambo yanayo husu watu wenye ulemavu. Pia inalenga kutoa elimu kwao na kwa jamii juu ya haki zao na kuongeza ufahamu juu ya uungwaji mkono kwa ajili ya utu, heshima na ustawi wao. Historia inaonyesha watu wenye ulemavu walikua na wakati mgumu zaidi kwa miaka iliopita. Kwakile kinachooeleza kua walikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutelekezwa na kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo ya kuishi. Hivyo uwepo wa siku hii ni kuthamini na kuenzi utu na heshima ya watu wenye ulemavu ambavyo vilitiwa kapuni kwa miaka mengi. Hivyo Disemba 3 ni wito wa kukumbatia utofauti wa kimaumbile tulio nao, kuvunja vizuizi na kuhakikisha mustakbali uliojumuishi zaidi kwa watu wote. Ikizingatiwa kwamba takribani watu bilioni 1.3 d...