NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ‘’TUMESHAWAHI kusimamisha shughuli ya harusi kwa dakika 10, mke asichukuliwe, baada ya kugundua hatujamtia pambo la kipini cha pua,’’anasema Rehema Faki Shehe (60) wa Kwale Micheweni Pemba. Ilishazoelekea kuwa, kuwa mapambo ni aina ya mafuta, podari, pete, mkufu, udi, wanja na hina, ingawa kwa wanawake wilaya ya Micheweni, kipaumbele ni utoboaji wa pua kwa ajili ya utiaji wa kipini. Utamaduni wa utoboaji (utomoaji) wa pua tena ya upande wa kushoto, wenyewe wanawake wa Micheweni waliurithi zaidi ya miaka 200 iliyopita. Kwa mfano, Rehema Faki Shehe (60) alimkuta bibi yake wakati akiwa huo akiwa na miaka 50, akiwa ametobolewa tundu la upande wa kushoto ya pua, akiwa na kipini. KINA MAAGA GANI KIPINI CHA PUA? Sharifu Massoud Hamad (60) wa Kwale Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, anasema moja ni tofauti kati ya mwanamke na mwanamme. Anaona hata unapokuta wamevaa mavazi yenye kufanana, lakini dalili kubwa ya tofauti hiyo...