Joyce Joliga,Songea
Tunduru. BARAZA la Madiwani Haashauri ya wilaya ya Tuneueu limeiomba Wizara ya afya kutoa elimu kufuatia kuzuka kwa homa ya kuharisha na kutapika kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambapo tayari watoto 41 wamelazwa na mmoja amefariki dunia .
Ombi hilo limetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Hailu Mussa,kufatia Diwani wa kata ya Nakayaya Daud Hamlima Mpendwa wakati akichangia hoja ya kamati ya huduma za jamii, Afya ,maji na elimu kwenye kikao cha baraza la kawaida kilichotokea kwenye ukumbi wa Klasta ya walimu wa tarafa ya mlingoti mjini hapa.
Akifafanua taarifa hiyo Mpendwa alisema kuwa amelazimika kutoa taarifa hiyo ili kuwakumbusha wataalam kutimiza wajibu wao kwa kufanya uchunguzi na kutoa majibu haraka kabla ya ungonjwa huo ulio ingia wa kuharisha kuathiri afya za wananchi.
Aidha, Diwani huyo amewaomba wataalamu kufanyia kazi na kudhibiti hali hiyo na kulitafutia majibu tukio hilo kabla ugonjwa huo haujaleta madhara makubwa kwa wananchi.
Akiongelea tukio hilo kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru Mussa Chaula alikiri kuwepo kwa matukio hayo na kwamba tayari mgonjwa mmoja mwenye umri chini ya miaka mitano ameripotiwa kufariki Dunia kutokana na ugonjwa huo .
Alisema tukio hilo lilianza kujitokeza mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu na tayari timu ya Wataalam ngazi ya mkoa na Wilaya walifanya ufutiliaji huo kwa kuchukua sampuri kutoka kwa wagonjwa 15 toka kwa watoto 24 waliolazwa hospitali ya wilaya,na watoto 17 waliolazwa hospitali ya misheni Mbesa.
Alisema mbali na chukukua sampuli hizo walienda katika kituo cha afya Mchoteka,watoto Mbesa ambako kulikuwa na watoto zaidi ya 40 ambapo zilichukuliwa kwa ajili ya kwenda kuoteshwa na waliendelea na matibabu.
Alisema oktoba 22 mwaka wataalamu kutoka ngazi ya mko 6 ilirudisha majibu kwamba hawakuona kitu na baadae sambuli hizo kupelekwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wizarani ambapo wanasubiri majibu.
Alisema katika kudhibiti hali hiyo tayari wameanza kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na kuwaasa akina mama wenye watoto wadogo kuwa waangalifu na mazingira wanayo cheza watoto wao,kunawa mikono na kuhakikisha wanaosha matunda kwa maji safi.
Comments
Post a Comment