Na Mwandishi Wetu@@@@ Kuelekea wiki ya Mwananchi, Mashariki wa klabu ya Yanga wa Kijiji cha Buma kilichopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamejitokeza kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ikiwamo madawati. Mashabiki hao walikabidhi madawati hayo katika shule ya Msingi Buma iliyopo kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa kutoa misaada kwa jamii kuelekea siku ya Mwananchi inayotarajiwa kufanyika Agosti 4 Mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa maarufu 'Lupaso'. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Tawi la Buma Ismail Omary amesema kuwa, wanachama wamekua na utaratibu wa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, lengo ni kurudisha hisani kwa wananchi wanaowazunguka kutokana na mwendelezo mzuri wa timu yao. " Leo tumejitokeza kwenye viwanja vya shule ya msingi Buma lengo ni kutoa msaada wa madawati ili wanafunzi waweze kuyatumia wakati wa masomo, huu ni utaratibu wetu wa kurudisha fadhira kwa wananchi kutokana na hamasa tunqzozipata za tim...