NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR@@@@ WAKULIMA wanaojishughulisha na kilimo cha mboga mboga, matunda na viungo kupitia MRADI wa VIUNGO (AGRI-CONNECT) wamekabidhiwa vifaa vitakavyowasaidia kuongeza nguvu katika uzalishaji wa bidhaa bora zitakazokidhi masoko. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliofanyika katika jengo la Kificho Mwanakwerekwe Meneja Mkuu wa mradi huo Simon Makobe alisema vifaa hivyo vitatumika kusaidia kuongeza uzalishaji na kufikia malengo ya utekelezaji wa mradi huo. Alisema MRADI wa VIUNGO ulilenga mambo mbalimbali ikiwemo kufungua fursa na kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao hapa Zanzibar pamoja na kupatiwa vifaa kwa lengo la kuwawezesha wakulima kuwa na nyenzo muhimu ili kulima kilimo bora kitakachowasaidia kujikwamua kiuchumi,”alisema. “Ugawaji wa vifaa hivyo ni moja ya mikakati ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na kutumia ujuzi mulioupata juu ya matumizi ya teknolojia muliyojifunza kipindi chote cha utekelez...