NA HAJI NASSOR, UNGUJA@@@@ KATIBU Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan, amesema njia nzuri ya kufanyakazi kwa jumuiya za wasaidizi wa sheria, ili kupata mafanikio, ni kuondokana na umimi wakati wa utekelezaji, wa shughuli zao. Alisema, wafadhili wanapotoa fedha zao, wanataka kuona matunda ya kilichofanywa na taasisi husika, sasa njia nzuri ni kushirikiana, wakati wanapotelekeza miradi hiyo. Katibu Mtendaji huyo aliyasema hayo jana, ukumbi wa mikutano wa Michenzani Mall mjini Unguja, wakati akichangia mada ya namna bora, ya kupata mafanikio, kwa watoa msaada wa kisheria, kwenye jukwaa la nne la msaada wa kisheria Zanzibar. Alisema, kama jumuia zitaendeleza na umimi na kujifungia ndani, wakati wanapotekeleza miradi, inaweza kuwa vigumu kupata mafanikio, yaliokusudiwa. Alieleza kuwa, jumuia za watoa msaada wa kisheria, zimekuwa zikifanyakazi moja kubwa, ingawa shida iliyopo ni kutoshirikiana wakati wanapofanyakazi hizo. ‘’Kwa mfano, jumuia ya wasaidizi wa she...