NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ HATIMAE mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto wa miaka saba, ambaye ni Askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba H.5290 D/C Godfrey Meckioru Mushi miaka (34) wa Limbani Wete, ameachiwa huru na mahkama ya mkoa iliyopo, Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Akitaja sababu za kuachiwa huru mtuhumiwa huyo Hakimu wa Mahkama hiyo Zuwena Mohamed Abdul-kadir alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, umekua dhaifu, na pia umeshindwa kuleta mashahidi muhimu. Alisema jumla ya mashahidi wanne walisikilizwa, ingawa ushahidi wao haukuweza kuishawishi mahkama, na kuweza kumtia hatiani mtuhumiwa. Alisema upande wa mashataka hawakuleta shahidi ambae ni baba mzazi wa muathirika, ambae yeye ndie aliemuhoji na kumuambia kama, mtuhumiwa ndie aliemfanyia kitendo hicho. ‘’Mahkama imepata wasiwasi na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe, kwamba ni wa kupangwa,’’alieleza. Alifahamisha kwa kutokana na mazingita hayo, mahkama haikumtia hatiani, hivyo imemuachia hu...