NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI kisiwani Pemba, waetakiwa kuipiga nambari 119, ambayo ni bure, wanapoona kuna viashiria au mtumiaji, muuzaji, msambaazaji na muingizaji wa dawa za kulevya nchini. Ushauri huo umetolewa leo Juni 13, 2026 na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maryam Juma Abdalla ‘ MABODI’ , wakati akizungumza na wananchi hao, uwanja wa Gombani Chakechake, kwenye uzinduzi wa siku ya kimataifa ya kupinga dawa za kulevya. Alisema, kwa upande wake serikali imeshaweka mikakati kadhaa, ikiwemo kuanzisha nambari hiyo bure kwa ajili ya kupokea taarifa, za dawa za kulevya. Alieleza kuwa, nambari hiyo iko wazi saa 24, na wananchi watakaoipiga watapokelewa na kupewa ushirikiano, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya. ‘’Tukiwa ndani ya uzinduzi wa kampeni ya kupinga matumizi, usambaazaji, uingizaji, uuzaji wa dawa za kulevya, leo itumie nambari hiyo bure, ili kuwaokoa vijana wetu,’’alisisitiza. Aidha Katibu Mkuu huyo, alisem...