NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NAIBU Waziri Mkuu, ambae pia ni Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Doto Mashaka Biteko, amesema kitendo cha kufanyika kwa mapinduzi ya Zanzibar, kilikuwa chema, kwani kililenga kuwapa uhuru wa wananchi, kusafiri nje ya mipaka kadiri wapendavyo. Naibu Waziri huyo Mkuu, aliyasema hayo Disemba 6, mwaka 2024 uwanjwa wa Umoja ni nguvu Mkoani Pemba, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi, wa ofisi na makaazi ya maafisa wa Uhamiaji, wilayani humo, ikiwa ni shamra shamra za miaka 60 ya mapinduzi. Alisema, mapinduzi hayo, yalikuwa yanafaa mno kuona wazanzibari na wananchi wote, wanatumia haki yao kwenda watakako kwa mujibu wa sheria, uhuru ambao hawakuwa nayo, kabla ya mapinduzi. Alieleza kuwa, mapinduzi hayo kupitia viongozi na wakuu wa nchi tokea mwaka 1964 hadi leo, wanaendelea kusimamia haki hiyo, ili kuhakikisha wananchi, wanasafiri zaidi nje ya mipaka ya Tanzania. ‘’Kila mmoja ni shahidi, baada ya kufanyika kwa mapinduzi ha...