NA HANIFA SALIM, PEMBA RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kila mwenye uwezo anawajibu wa kutoa sadaka kwa kuwasaidia ambao hawana uwezo hususani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Alisema katika mwezi huu mtukufu wafadhili wengi wamejitoa katika kuwasaidia watu ambao wana hali duni za kimaisha, hivyo aliwataka wananchi wenye uwezo kujitolea kutoa sadaka kwa wenzao ambao wako katika mazingira magumu. Aliyasema hayo kwa nyakati tofauti, katika hafla ya kukabidhi msaada wa futari kwa wazee, mayatima, wajane na watu wenye ulemavu kwa Mkoa wa Kusini Pemba, iliyofanyika ofisi ya Mkuu wa wilaya Mkoani na Tibirinzi Chake chake. "Ni kweli wanaopata ni wachache na wanaohitaji ni wengi, lakini hii ni taasisi moja tu zipo na taasisi nyengine ambazo zimesaidia, ikiwemo kampuni ya Olympic na mashirika mengi yamesaidia kwa Wilaya ya Micheweni na Wete", alisema. Dk. Mwinyi alisema, kwa niaba ...