Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ELIMU

MKURUGENZI TUJIPE: ‘ELIMU KIDATO CHA NNE BADO NDOGO JIENDELEZENI'

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAHITIMU kidato cha nne skuli ya sekondari Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, wamekumbushwa kuwa, elimu waliyoipata bado ni ndogo, hasa kwa ulimwengu ulivyo, na badala yake, watafute namna ya kujiendeleza. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba ‘TUJIPE’ Tatu Abdalla Msellem, kwenye mahafali ya 18 ya wanafunzi hao, yaliofanyika skulini hapo. Aliwaambia wahitimu hao kuwa, kwa sasa elimu imeongezeka thamani, na ndio maana kidato cha nne ni kama mwanzo wa kutafuta elimu, hivyo wahakikishe wanashirikiana na familia zao, ili kujisomea zaidi. Alieleza kuwa, kwa sasa kuanzia kidato cha sita na kuendelea, ndio mwanzo wa elimu, hivyo kwa wale wanafunzi ambao hatobahatika kuendelea kidato cha tano na sita, wasivunjike moyo. ‘’Elimu ya kidato cha nne, kama ndio mwanzo wa elimu kwa dunia ya sasa, na wale ambao hawatobahatika, bado nafasi ya kujiendeleza kimasomo wanayo,’’aliwakumbusha. Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ‘TUJIPE’ aliwasisit...

MIAKA MINNE YA DK. MWINYI: KONDE WAPATA SKULI YA GHOROFA TATU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema ameshayatekeleza kwa vitendo, aliyowaaahidi wananchi, ikiwemo ujenzi wa madarasa 2,773 katika skuli zote za Unguja na Pemba. Alisema, Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliitaka serikali kujenga madarasa 1,500 ingawa wameshavuuka lengo hilo, kwa asilimia 184, na bado kazi inaendelea. Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana, mara baada ya kuifungua skuli ya skondari ya ghorofa tatu ya Konde wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ikiwa ni shamra shamra za miaka minne ya uongozi wake. Alisema, serikali imepanga hadi kufikia mwaka 2025, iwe imeshajenga vyumba 2,000 vya madarasa katika skuli zote za Unguja na Pemba, ili kuondoa mikondo miwili. Alisema kama kuna watu wanapiga porojo na kusema, uongo waangalie takwimu kutoka wizara ya elimu, zitadhihirisha ahadi zake kwa wananchi. Akizungumza mafanikio mingine, alisema ni kuongezeka kwa bajeti ya mikopo ya elimu ya juu...

DK. MWINYI AFYEKA MSONGAMANO WA WANAFUNZI MWAMBE, ASHUSHA GHOROFA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ILIKUA kama ndoto, kwa siku ya kwanza kati ya zile 360 zinazounda mwaka. Ndoto hizi zilikuwa kwa waalimu, wanafunzi, wazazi, walezi wa shehia ya Mwambe Mkoani Pemba, kunawa uso mbele ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi. Sio tu kunawa uso, kwa maji kama ilivyozeeleka, wao walinawa kwa kumalizika skuli ya msingi ya ghorofa mbili eneo hilo la Mwambe. Hapa wazazi, walezi, wanafunzi na waalimu, maji kwenye upindo wa kucha ya mtoto mchanga, yalitosha kuwakogesha mwili mzima. Furaha yao, sio tu kuamka wakiwa wazima siku hiyo ya Januari 1, mwaka 2023, lakini ni pale waliposhuhudia jengo la kwanza la ghorofa katika eneo la Mwambe, na bahati nzuri sio la mtu binafsi, bali likiwa la serikali. WANANCHI MWAMBE Haji Omar Kheir (65), anasema aliposikia ahadi ya rais wa sasa wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, juu ya ujenzi wa skuli ya ghorofa, hakuamini. ‘’Si unajua baadhi ya wanasiasa wakitaka jambo lao, watakuahidi jambo hata ambalo yeye hajawahi...