NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ABRAHMAN Juma Abdalla miaka 70, mkaazi wa kijiji cha Kuyuni wilaya ya Mkoani, ameanguka ghafla na kufariki dunia papo hapo, akiwa kwenye foleni ya kuchukua maji ya kiimani katika bahari ya Msuka, wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba. Itakumbukuwa kua, eneo hilo lilishafukiwa na kupigwa marufuku na serikali, kuwataka wananchi wasiyatumie maji hayo, kwa kutokuwa salama kiafya. Pamoja na marufuku hiyo, imeabainika kuwa wapo baadhi ya wananchi, wamekuwa wakilitumia eneo hilo na kuchota maji ya kiimani, yanayodaiwa kuponyesha magonjwa na maradhi sugu. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walisema mpatwa na mauti, alifika shehia ya Msuka mashariki leo Mei 6, mwaka huu majira ya saa 3:00 asubuhi, akitokea kijijini kwao Kuyuni wilaya ya Mkoani. Walisema, mzee huyo alifika eneo hilo, akikabiliwa na magonjwa sugu, ili kuchukua maji hayo, ambayo alikuwa anaamini, yanaweza kumponyesha magonjwa yake. Mmoja kati ya mashuda hao Omar Kije Omar alisema, mzee huyo