Skip to main content

Posts

Showing posts from December 1, 2024

MKURUGENZI TUJIPE: ‘ELIMU KIDATO CHA NNE BADO NDOGO JIENDELEZENI'

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAHITIMU kidato cha nne skuli ya sekondari Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, wamekumbushwa kuwa, elimu waliyoipata bado ni ndogo, hasa kwa ulimwengu ulivyo, na badala yake, watafute namna ya kujiendeleza. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba ‘TUJIPE’ Tatu Abdalla Msellem, kwenye mahafali ya 18 ya wanafunzi hao, yaliofanyika skulini hapo. Aliwaambia wahitimu hao kuwa, kwa sasa elimu imeongezeka thamani, na ndio maana kidato cha nne ni kama mwanzo wa kutafuta elimu, hivyo wahakikishe wanashirikiana na familia zao, ili kujisomea zaidi. Alieleza kuwa, kwa sasa kuanzia kidato cha sita na kuendelea, ndio mwanzo wa elimu, hivyo kwa wale wanafunzi ambao hatobahatika kuendelea kidato cha tano na sita, wasivunjike moyo. ‘’Elimu ya kidato cha nne, kama ndio mwanzo wa elimu kwa dunia ya sasa, na wale ambao hawatobahatika, bado nafasi ya kujiendeleza kimasomo wanayo,’’aliwakumbusha. Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ‘TUJIPE’ aliwasisit...