Skip to main content

Posts

Showing posts from October 1, 2023

MRADI WA ‘SWIL’ ZANZIBAR, ULIVYOWAONESHA NJIA WANAWAKE KUDAI HAKI ZAO: TAMWA, PEGAO ZASEMA JAMBO

                  NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@  HAWAKUKOSEA waliosema 'umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu' Msemo huu umesadiki katika utekelezaji wa mradi wa kuwawezesha wanawake kudai haki zao za uongozi , demokrasia na siasa 'SWIL' unaotekelezwa kwa mashirikiano kati ya   TAMWA Zanzibar, ZAFELA na PEGAO. Mradi huo ambao ulizinduliwa mwaka 2020 na kutarajiwa kumalizika 2023 umeonekana na mafaniko makubwa katika hatuwa mbalimbali za utekelezaji wake. Utekelezaji wa mradi huo ambao ulitarajiwa kuwafikia na kuwawezesha wanawake 6000 kwa zanzibar, Unguja na Pemba katika kudai haki zao ili nao waweze kuwawezesha wengine tayari umeonyesha njia katika kufikia hatuwa ya kudai haki zao za uongozi.   Mradi huo wa SWIL ambao unafadhiliwa na ubalozi wa Norway umetekelezwa maeneo mbalimbali ambapo kwa upande wa   Pemba tayari     umeshawafikia wastani wa wanawake 4000.   Katika hatuwa za kufanikisha lengo la mradi la kuwawezesha wanawake kudai haki zao za uongozi