HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE RIZIKI PEMBE JUMA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUTOA TAARIFA YA KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA “MTOTO MBONI YANGU”, SIKU YA TAREHE 25/10/2024 KATIKA UKUMBI WA WIZARA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO - KINAZINI ZANZIBAR NDUGU WAANDISHI WA HABARI ASSALAMU ALAYKUM. Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia neema ya uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana siku ya leo kwa ajili ya kutoa taarifa ya KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA MTOTO MBONI YANGU. NDUGU WAANDISHI WA HABARI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya “Ndoto Ajira” kutoka Dar es Salaam imeandaa kampeni ya kitaifa yenye jina la MTOTO MBONI YANGU , ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Zanzibar. Lengo kuu la kampeni hii ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuizunguka nchi nzima ya na kuielimisha, kuiasa na kuzung...