Skip to main content

Posts

Showing posts with the label WATUMISHI WA UMMA

''MSITEGEMEE WANGANGA WA KIENYEJI KUPANDA VYEO, CHAPENI KAZI'

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKURUGENZI Baraza la Manispaa ya Chake chake Maulid Mwalim Ali, amewataka watumishi wapya wa umma kisiwani Pemba, kutotegemea waganga wa kijienyeji, kutafuta vyeo katika ofisi zao, na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwani ndio msingi mkuu. Alisema, huu sio wakati tena wa kuelekea kwa wapigamrali, ili kusaka vyeo, bali mchawi wa hilo ni kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi na bila ya ubaguzi. Mkurugenzi huyo aliyasema hayo jana, ukumbi wa Manispaa hiyo alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wapya wa umma, kuhusu uthibitisho wa kazi baada ya kuajiriwa. Alisema, nidhamu, utendaji kazi uliotukuka, heshima na kutoa huduma bora, ndio chanzo cha wao kupanda daraja katika maeneo yao ya kazi. ‘’Niwaombe sana watumishi wenzangu wa umma, kuhakikisha mnakwenda kufanyakazi kwa bidii na nidhamu, kwani huo ndio msingi mkuu wa kupanda daraja,’’alifafanua. Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo, amewataka watumishi hao wapya, kujenga umoja n...