NA MWANDISHI MAALUM-ZANZIBAR Katika juhudi za kuimarisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na kukuza haki za kidemokrasia, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA- ZNZ) kimetoa mafunzo ya siku mbili kwa Wahamasishaji Jamii (Citizen Brigades) wapatao 60 kwa upande wa Unguja ikiwa ni sehemu ya programu ya kuimarisha uongozi kwa wanawake (SWIL) wenye lengo la kujenga jamii yenye usawa wa kijinsia kwa kuwawezesha wanawake kushika nafasi katika ngazi za maamuzi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TAMWA ZNZ, Saphia Ngalapi, ameeleza kuwa watekelezaji wa programu wana imani na wahamasishaji waliopatiwa mafunzo na kuwa watakuwa mabingwa wa kuhamasisha jamii juu ya haki za wanawake kushiriki katika uongozi. "Kupitia timu hii, tunatarajia mabadiliko katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki ya demokrasia na uongozi kwa wanawake ili kufikia 50% kwa 50% katika ngazi za maamuzi, jambo litakalochangia kuleta maendele...