Skip to main content

Posts

Showing posts with the label WANANCHI UWANDANI

WANANCHI UWANDANI WAKIPA ‘KONGOLE’ ZLSC

   NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake, wamesema kambi ya siku tatu ya kutoa ushauri na msaada wa kisheria, inayoendeshwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, imezaa matunda kwao, kwa kupata ufumbuzi baadhi ya changamoto za kisheria, ikiwemo mirathi. Wakizungumza na blog ya Pemba today, leo April 14, 2025  kwenye kambi hiyo skuli ya Uwandani, walisema wamepata ufumbuzi mkubwa, ambao baadhi yao walishakata tamaa. Mmoja wa wananchi hao, aliyekataa kutaja jina lake, alisema tatizo lake la mirathi wa mali kadhaa, umepatiwa ufumbuzi wa haraka, baada ya kuitwa upande anaoulalamikia. Nae Riziki Abdalla Suleiman (29), ambae alilalamikia kukosa vitambulisho vya mkaazi, cha taifa na cheti cha kuzaliwa, sasa amepata muelekeo. ‘’Nilishahangaika kwa zaidia ya miaka 19, lakini sijafanikiwa, ingawa kupitia ushauri wa kisheria uliotolewa na ZLSC, sasa nimeondoka na furaha,’’alieleza. Kwa upande wake Mwana Said Khamis (30), alieleza kuwa,...