NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MWALIMU Mkuu wa skuli ya sekondari ya Connecting Continent, iliyopo Mgogoni wilaya ya Chake chake Pemba, Mwache Juma Abdalla, amewataka wanafunzi wa darasa la kumi na mbaili skulini hapo, kuzitumia kwa maandalizi ya hali ya juu, wiki 11 zilizobaki, kabla ya kufanya mtihani wao wa taifa. Alisema, wiki hizo sio kidogo, kwa mwanafunzi kama ataweka pembeni uvivu, kudorora, kushughulikia anasa na kujikita kwenye masomo, hivyo anaweza kufanya vizuri, kwenye mtihani wa taifa. Mwalimu mkuu huyo, aliyasema hayo leo Augost 24, 2024 skulini hapo, kwenye kikao cha wazazi na wanafunzi hao, cha kutoa matokeo ya mitihani ya majaribio ya kimkoa ‘MOCK’ yaliofanyika hivi karibuni. Alisema, bado wanafunzi wanayonafasi ya kujiandaa na mitihani hayo, kwani waalimu wameshamaliza mtaala waliopangiwa, na sasa ni kazi wanafunzi wenyewe. Alieleza kuwa, waalimu wamekuwa wakitumia jitihada binafsi ili kuhakikisha wanamaliza mitaala mapema, na sasa ni kazi ya wanafunzi kuang