NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WADAU wa haki za binaadamu kisiwani Pemba, wamegundua kuwa Zanzibar inazosheria, kanuni na sera nzuri kwa ajili ya watu wa wenye ulemavu, ingawa changamoto kubwa ni utekelezaji wake kwa vitendo. Walisema, kwa mfano ipo sheria na sera, inayotaka kila jengo la umma, liwe ni njia maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu, ingawa changamoto ni kutotekelezwa na mamlaka wakati wa ujenzi. Wakizungumza kwenye kikao kazi, kilichoandaliwa na Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ chenye lengo la kupitisha changamoto za kisheria kwa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana, kilichofanyika leo Disemba 16, 2023 skuli ya maandalizi Madungu Chake chake. Walisema, hata suala la ajira kwa kundi hilo, limewekwa katika sheria kama ilivyo suala la haki nyingine za kibinaadamu, ingawa shida ni utekelezaji wake. Mmoja kati ya wadau hao, Khalfan Amour Mohamed kutoka Jumuiya kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili ‘ZAPDD’ Pemba, alisema inashangaaza kuona majengo ya um