NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAAFISA mawasiliano na habari wa Jumuia za wasaidizi wa sheria Tanzania zimetakiwa kujenga ushirikiano wa karibu na watendaji wenzao, ili kuhakikisha wanakuwa na mifumo sahihi ya utoaji wa taarifa za jumuia. Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa masoko kutoka LSF Gilsant Mlaseko, wakati akizungumza na maafisa hao kwenye mkutano wa kujengewa uwezo kwa njia ya kielektroniki. Alisema bidhaa ya mwasiliano sio haki ya Afisa Mawasiliano na Habari pekee kwenye jumuiya, bali anatakiwa kuwa karibu na wakurugenzi, waratibu na watendaji wengine. Alieleza kuwa, wakati mwingine ndani ya Jumuiya Afisa huyo anaweza kuwa mwisho katika utoaji wa taarifa na hasa baada ya kuidhinishwa na kuthibitishwa na kamati iliyoteuliwa. ‘’Suala la mawasiliano hasa ya kutoka nje ya Jumuiya, linapaswa watoa taarifa wawe makini na sio jukumu la mtendaji mmoja, bali iwe ni timu ya Jumuiya na kisha muhusika anateuliwa,’’alieleza. Akieleza umuhimu wa mawasiliano Mtaalamu huyo, a...