NA HANIFA SALIM, PEMBA WAANDISHI wa habari ni watu muhimu katika jamii yoyote ile ulimwenguni. Maana moja ya majumku yao ambayo sio rahisi kufanya na kundi jengine la watu ni kule, kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha iwe kijamii, kisiasa,kiutamaduni na kiuchumi. Licha ya changamoto ambazo wanakumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao, bado wana dhima kubwa ya kuipatia jamii taarifa ambazo zinatokezea kila siku. Pamoja na kadhia hiyo taasisi kama hizo za vilabu vyao, ‘Press Club’ huwa zinasimama wima, kuwatetea waandishi hao wanaokumbwa na madhila kadha. Mei 3 ya kila mwaka duniani kote, kunaadhishwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari, ni siku muhimu kwa waandishi wa habari. Waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi zao kwa mujibu wa katiba zote mbili, ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Zanzibar ya mwaka 1984 ambazo zinahimiza upatikanaji wa habari na kutowa habari kwa wananchi. Kwa kawaida kila jambo ambalo linamaslahi na watu ili liw