NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SASA ni miaka 26 tokea kuasisiwa kwa sheria ya Tume ya Utangaazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997, licha ya kujumuisha na marekebisho yake. Sheria hii, imekuja kusimamia, kuangalia mwenendo wa vyombo vya habari Zanzibar hasa redio, televisheni na vile vya kisasa vyenye kurusha maudhui yao mtandaoni. Sheria hii yenye vifungu 30, vilivyobebwa na sehemu sita kuu, inavyovifungu kwa hakika sio rafiki, kuelekea uhuru kamili wa habari hapa Zanzibar. SHERIA KWA UJUMLA Kama ilivyo sheria nyingine zote, kwenye sehemu ya kwanza imeundwa na vifungu vitatu, maana kile cha nne, kimefutwa na kati ya hivyo kimoja kinatoa jina la sheria na maana ya maneno. Kwa mfano, mtangaazaji ni mtu ambaye amepewa leseni chini ya sheria hii ya kutoa huduma za utangaazaji katika vyombo vya habari. Kwenye sehemu ya pili ya sheria hii, yenyewe imeundwa na vifungu kuanzia cha tano (5) hadi cha 10, na kubwa zaidi lililopo ni pamoja na uanzishwaji wa Tume ya Utangaazaji Zanzibar. Je...