NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa vijiji vya Tironi na Kionwa, wilaya ya Mkoani Pemba, wameikumbusha wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, kuwafikiria ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha lami, iliyoanzia Mbunguwani. Walisema, wanaona wivu mkubwa kuona zipo barabara za ndani, kwa sasa zinaendelea na ujenzi, ambao yao haijaanza hata kupimwa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema wakati umefika kwa sasa, kwa wizara husika, kuwatupia jicho, ili waondokane na usumbufu hasa kipincdi cha mvua. Walisema, barabara yao imekuwa ikitoa kwa wingi zao la taifa la karafuu, hivyo ni vyema sasa mapato ya nchi hii, yakaelekezwa kwao, kwa ujenzi wa barabara yao. Mmoja kati ya wananchi hao Maryam Haji Khamis, alisema wamekuwa wakipata dhiki, hasa wanapopata uhamisho wa kimatibabu. āāKwa mfano sisi wazazi, wakati mwingine tunahitajika kwenda kirufaa hospitali ya wilaya ya Mkoani, lakini usumbufu, ni uwepo wa barabara iliyochakaa,āāalieleza...