NA MWANDISHI WETU, PEMBA JAMII kisiwani Pemba, imetakiwa kufahamu changamoto na viashiria vya udhalilishaji kwa watoto, ili kuwalinda na vitendo hivyo. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Pemba ‘PACSO’ Mohamed Ali Khamis, mara baada ya kuutambulisha mradi wa kujadili changamoto zinazowakabili watoto, katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake Pemba. Alisema, jamii inapaswa kuwa karibu mno na watoto wao, ili kujua haraka viashiria vya kudhalilishwa, na sio kusubiri hadi janga liwakumbe. Mwenyekiti huyo alieleza kuwa, hilo litakuwa rahisi ikiwa wazazi na walezi watatenga muda wa kuwa karibu na watoto wao. ‘’Kama tunajiona tuko na harakati nyingi za maisha na kusahau kukaa na watoto wetu, wanaweza kukumbwa na janga kama la udhalilishaji na tukachelewa kufahamu,’’alieleza. Akielezea lengo la mradi huo Mwenyekiti huyo wa PACSO, alisema ni kuwazindua wazazi, kufahamu viashiria na changamoto na namna ya kuwasaidia watoto was