NA SALMA LUSANGI, ZANZIBAR WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Zanzibar 'ZECO' wameahidiwa kuwa watafukuzwa kazi, endapo uchuguzi unaoendelea ukibaini wameshiriki katika kuwaunganishia umeme watu waliyokamatwa kwa kosa la kujiunganishia, umeme kinyume na sheria Zanzibar. Kauli hiyo imeitowa na Katibu Mkuu wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi wakati akizungumza na watendaji wa ZECO, katika ofisi ya shirika hilo jana. mjini Zanzibar. Alisema mwananchi wa kawaida aliyekuwa hajasoma fani ya umeme, hawezi kuchezea umeme lazima alishirikiana na mtaalamu wa umeme kutoka ZECO au nje ya ZECO hivyo ripoti ya uchunguzi ikionesha mtendaji wa Shirika amehusika atamfukuza kazi. “Mimi ninavyofahamu nguzo ya umeme haikai ndani ya fensi, kuna mtu hapo amecheza aidha kuungana na mfanyakazi wa ZECO na mfanyakazi yeyote aliyeshiriki kuungana na kishoka hatakuwa salama nitamchomoa,''alieleza. Aliwanasihi wafanyakazi hao, wakati huu ni vizuri ajitokeze mwenyewe ili ajulikane aliye