NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa Divisheni ya Katiba na Sheria Pemba Bakari Omar Ali, amewasisitiza wasaidizi wa sheria, kukumbuka kuwa , bado dhana ya kujitolea kwa aina ya kazi yao hiyo, itabakia pale pale licha ya changamoto walizonazo. Alisema, kwa mujibu wa sheria inayowaongoza, ni kosa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria na kisha kuomba malipo kwa m wananchi husika. Mkuu huyo wa Divisheni, aliyasema hayo leo Febuari 09, 2025 ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ wakati akitoa maoni yake, baada ya kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti kwa wasaidizi wa sheria , kisiwani humo. Alisema, ijapokuwa sasa wapo wanaodai malipo kama baraka ya kufanyakazi zao, lakini bado sheria haitambuwi uwepo wa posho kama motisha wa kufanya kazi zao. Alieleza kuwa, msingi mkuu wakati wa lipo omba kazi hiyo na sasa ikiingizwa ndani ya sheria yao, ni kufanyakazi kwa njia ya kutolea, na hasa kwa wananchi wanyonge na makundi maa...