NA MWANDISHI WETU, PEMBA MKUU wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, ameuhakikishia, uongozi wa mbio za mwenge kitaifa wa mwaka 2025, kwamba watayafanyia kazi maagizo, maelekezo na ushauri waliutoa, hasa suala la kutunza amani na utulivu, kuelekea uchaguzi mkuu . Mkuu huyo wa wilaya aliysema hayo jana, eneo la skuli ya Ngwachani wilayani humo, kwenye hafla ya kumkabidhi mwenge huo, mwenzake wa wilaya ya Chake chake Mgeni Khatib Yahya. Alisema ujumbe wa mwenge kiujumla, umekuja kuwazindua wananchi wa wilaya yake, juu ya umuhimu wa kutunza amani, kwa maslahi mapana ya taifa na watu wake. Alieleza kuwa, wakati mwenge huo unakimbizwa wilayani mwake na kukutana na wananchi, ulisisitiza utunzaji wa amani, na hasa kuelekea mwezi Oktoba mwaka huu, kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi. Dk. Hamad alifahamisha kuwa, jingine ambalo mwenge huo wa uhuru chini ya kiongozi wake Ismail Ali Ussi, ulisisitiza, ni kupiga vita dawa za kulevya ...