Skip to main content

Posts

Showing posts from June 28, 2026

KIZUNGUMKUTI TUHMA ZA UKATILI, UDHALILISHAJI KWA KIZIWI MICHEWENI

  SAIDA ALI, PEMBA MAMA mzazi ambae mwanawe mwenye ulemavu wa uziwi wa miaka 38, alifanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji, ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama, kuwa haki itendeke kufuatia unyama aliodai kufanyiwa, kijana wake. Aliyasema hayo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, shehia ya Shumba vyamboni wilaya ya Micheweni, kufuatia sitofahamu ya majibu ya hospitali na athari aliyonayo kijana wao. Alisema kuwa kitendo alichodai kufanyiwa kijana wao huyo, ambacho alimshuhudia akiwa amefungwa mikono nyuma akiwa na tambara mdomoni, ni cha kikatili na udhalilishaji. Alieleza kuwa, muda wa saa 8:00 usiku baada ya kusikia kelele za kukorota kwa kijana wake, alikimbilia chumbani kwake, na kufika alijonea maajabu. ‘’Kwanza alikuwa amevungwa mwiili mzima nguo nyeusi mithili ya beibui, nilishuhudia vichupa vidogo viwili, kimoja kikiwa na majimaji, (dawa) nusu na chingine kikiwa kitupu,’’alifafanua. Aidha mzazi huyo alisema, jingine ambalo limemshitua kwa kij...