NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa mkoa wa kaskazini Pemba, wametakiwa kuzitumia siku tatu za kambi ya kutoa masaada wa kisheria, ili kufikisha malalamiko yao ya kisheria, na kupatiwa ufumbuzi papo hapo. Hayo yameelezwa leo Oktoba 17, 2024 na Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, katika hutuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Wete Dk. Hamad Omar Bakari, kwenye uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, iliyozinduliwa uwanja wa Majengo Micheweni Pemba. Alisema, siku tatu hizo watakuwepo wanasheria, Jeshi la Polisi, wasaidizi wa sheria, mahakim na mawakili, ili kusikiliza changamoto za kisheria na kuzitolea ufumbuzi papo hapo. Alieleza kuwa, kuwapata wanasheria wakati mwingine huwa ni vigumu, ingawa kufuatia uzinduzi wa kampeni hiyo, wanapatikana papo hapo bila ya malipo. ‘’Niwatake wananchi wa mkoa wa kaskazini Pemba na hasa wa wilaya ya Micheweni, kufika hapa Micheweni majengo, ili kupata elimu na msaada wa kisheria tena ...