PICHA NA MTANDAO SIO HALISI YA VIZIWI NA HAJI NASSOR, PEMBA ULEMAVU ni upungufu wa uwezo wa viungo vya mwili, akili au hisi unaomsababishia mtu, kushindwa kumudu mazingira yake au kushindwa kushiriki kikamilifu katika kazi za kijamii. Ndivyo ilivyoa toa tafsiri ya nini maana ya ulemavu, sheria ya watu wenye ulemavu (haki na fursa ) ile namba 9 ya mwaka 2006 ya Zanzibar ielezavyo. Sheria hii ikaenda mbali zaidi na kufafanua kuwa, ulemavu unaweza kuwa wa kudumu au wakati mwengine ni wa muda, huku baadhi ya magonjwa kama vile ya akili yanaweza kusababisha ulemavu pia. Tendo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutunga sheria hii, ni kuona umuhimu na ulazimu ule uliomo kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kwamba binadamu wote ni sawa mbele ya sheria. Kumb...