NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ WATUMISHI wapya wa wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Pemba, wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni za utumishi wa Umma ili kuongeza uwajibikaji katika utendaji wao. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Idara ya uratibu na Utumishi kutoka wizra ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Harith Bakari Ali, wakati akifungua mafunzo ya kuthibitishwa kazi kwa waajiriwa wapya yaliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Michakaini Chake chake Pemba. Alisema ufanisi wa kazi hutokana na kufuatwa ipasavyo kwa Sheria, miiko na maadili ya kazi ambayo humtengeneza mtumishi kua muawajibikaji katika utendaji wake wa kila siku ndani na nje ya eneo la kazi. "Sheria, maadili, kanuni na miiko ya kazi ndio kichocheo muhimu cha uwajibikaji kwa mtumishi wa Umma, hivyo ni muhimu kuyazingatia yote haya ili kufanya kazi zenu vizuri na si katikamaeneoyakazi tu bali hata nje ya kazi, alieleza. Alisema kua kipengele chengine muhimu ...