NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ KAMPENI ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan, imetangaazwa kwa wanafunzi wa skuli ya skondari ya Maziwang’ombe na wale wa Chuo cha kiislamu Micheweni. Wataalamu wa masuala ya kisheria kutoka ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka, Jeshi la Polisi, Mawakili wa kujitegemea, Maafisa ustawi wa jamii na wanasheria wa halmashauri, walifika leo Juni 1, 2025 kwenye kampeni maalum inayoendelea. Wakizungumza kwenye mikutano hiyo ya wazi, walisema kampeni hiyo inakuja kuwaelezea wananchi na hasa wanawake, watu wenye ulemavu, waliomo kwenye makundi maalum na wasiokuwa na uwezo, kujua haki na wajibu wao kisheria. Inspekta Saleh Ame Makame kutoka kituo cha Polisi Chake chake, aliwataka wanafunzi hao, kuripoti wanapoona viashiria vya udhalilishaji dhidi yao na wasivifumbie macho. Alisema, kama lengo la kampeni hiyo ni kuwaelezea haki na wajibu wao, hivyo wahakikisha wanawaripoti wanao...