NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKURUGENZI wa Baraza la Mjia Mkoani Muumini Abeid Salum, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika mashindani ya sita ya tahafidhil-quran, ya kanda ya Wambaa wilayani humo asubuhi ya kesho Machi 14, 2026. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa Jumuiya ya tahafidhil qur-an kanda ya Wambaa, Mwalimu Abdalla Haji Ali, alisema tayari maandalizi ya shughuli hiyo, yameshakamilika. Alisema, Mkurugenzi huyo, atawashuhudia wanafunzi wakishindana kwa juzuu ya kwanza, pili, tatu, tano, saba, 10 na 20, wakiwemo wanafunzi wa kike na kiume. Alieleza kuwa, mashindani hayo ya aina yake kwa mwaka huu, yanatarajiwa kufanyika msikiti wa Ijumaa Wambaa wilayani humo. Alisema, baada ya majaji kukamilisha kazi yao hiyo na kutoa matokeo, mgeni rasmi huyo atatoa zawadi ikiwemo fedha taslimu, kwa washindi na washiriki wote 45. ‘’Ni kweli asubuhi hii, Mkurugenzi wetu wa Baraza la mji la Mkoani, atayashuhudia mashindani ya sita ya tahafidhi qur-an, yanayoandaliwa ...