NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ‘…….SEA Cucumbers’ ama matango bahari…... Na wingine huliita jongoo la pwani, ama kiazi bahari. Ni aina ya wanyama ama kiumbe, kinachoendesha maisha yake baharini. Kitango bahari, kina ngozi ngumu kiasi na mwili mrefu ambapo muonekano na maumbile yake ni sawa na kitango kinacholiwa nchi kavu. Kitango bahari, kinaendelea kufafanuliwa kwenye vitabu na mitandao kuwa, kina mwili mrefu wenye via vya uzazi, moja iliyo na matawi. Wanyama hawa, wanapatikana kwenye sakafu za bahari duniani kote, wakiwa wamegawanyika kwenye spishi zaidi ya 1,717. Ingawa nyingi zao, zinapatikana eneo la Asia-Pasifiki, ambapo kwa Zanzibar utafiti umeonesha zipo zaidi ya aina 35. Vitango bahari, huishi kwa kutambaa kwenye sakafu ya bahari, na kuweka hifadhi na kujisitiri kwenye matumbawe. Maisha ya viumbve hawa, waliokua hawakuwa na thamani kwa zaidi ya karne moja Zanzibar, maisha yao yana mchango mkubwa katika ikolojia ya bahari, hasa katika kuisafisha. ...