NA HAJI NASSOR, PEMBA:::: MAPUNGUFU yaliyopo katika sheria mbali mbali Zanzibar, zimetajwa kuwa zinachangia kutokuwepo kwa uwiano wa usawa wa kijinsia, kati ya wanawake na wanaume katika ngazi mbali mbali za uongozi. Mapungufu ya sheria hizo yameibuliwa na wanajamii kufuatia mikutano 41 iliyofanyika katika shehia 44 kisiwani Pemba, iliyoandaliwa na wahamasishaji jamii kwa kushirikiana na asasi za kiraia kisiwani hapa, juu ya ushiriki wa wanawake katika kushika nafasi za uongozi na demokrasi. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyobainika kwenye sheria kukwaza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi, Mkurugenzi wa Jumuiya ya utetezi wa Jinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) Hafidh Abdi August 8, mwaka 2022, alisema miongoni mwa Asasi zilizoshirikiana kuchambua mapungufu hayo ni pamoja na taasisi ya Tumaini Jipya Pemba (TUJIPE), Nihurumie Foundation, KOK Foundation, PRADO, PACSO, Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu, pamoja na Kituo cha hudum